Kimataifa

Afisa mwingine wa upinzani Tanzania atekwa nyara na kupigwa uchaguzi mkuu wa 2025 ukikaribia

Na REUTERS, CHARLES WASONGA October 21st, 2024 Kusoma ni dakika: 1

DAR ES SALAMA, Tanzania

WATU wasiojulikana walimteka, kumcharaza na kumjeruhi vibaya kiongozi mmoja wa kike wa upinzani nchini Tanzania kabla ya kumtupa msituni.

Chama kikuu cha upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jumapili kilisema kuwa Katibu wa tawi lake la wanawake, Aisha Machano, alitekwa nyara katika mji wa Kibiti mashariki mwa nchi hiyo akiwa katika shughuli rasmi za kikazi.

“Wahudumu wa bodaboda walimpata katika hali mbaya kiafya huku awa na maumivu makali,” chama hicho kilisema kupitia ujumbe katika jukwaa lake la mtandano wa kijamii X.

Chadema ilisema waliomteka Machano walitaka maelezo kuhusu aliyewaagiza kuteketeza nguo zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kama zawadi kwa wanawake wakatu wa maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani katika eneo la Kilimanjaro.

“Alikimbizwa hospitalini kwa matibabu na amepelekwa katika chumba cha upasuaji kwa ukaguzi zaidi kiafya,” chama hicho kikasema.

Msemaji wa Polisi David Misime alisema baada ya kupokea habari kwamba Machano alipatikana katika msitu mmoja viungani mwa Kabiti, maafisa walianzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.

“Tunatoa wito kwa umma kudumisha utulivu kwani uchunguzi utatoa maelezo kuhusu kilichomtendekea, sababu ya tukio hili na watu waliohusika. Kisha tutachukua hatua kulingana na ushahidi uliopo,” akasema.

Bi Machano ndio afisa wa pili wa cheo cha juu wa chama cha Chadema kutekwa nyara na kuteswa ndani ya miezi miwili.

Mwezi jana Ali Kibao, mmoja wa maafisa katika sakritariati ya chama hicho, alitekwa nyara na watu wenye bunduki alipokuwa akisafiri kutoka Dar es Salama hadi mji wa Tanga.

Visa vya kutekwa nyara kwa viongozi wa upinzani vimeiharibu sifa ya Rais Samia Suluhu Hassan.