• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Hakuna thibitisho waliopona Covid-19 wana ‘kingamwili’ kuzuia maambukizi mapya – WHO

Hakuna thibitisho waliopona Covid-19 wana ‘kingamwili’ kuzuia maambukizi mapya – WHO

Na AFP

SHIRIKA la Afya Ulimwenguni (WHO) limetahadharisha kuwa wagonjwa ambao wamepona baada ya kuugua Covid-19 bado wanaweza kuambukizwa virusi vya corona kwa mara nyingi ikiwa hawatazingatia maagizo ya kuzua maambukizi.

WHO ilisema Jumapili kwamba kupona kutokana na ugonjwa huo hakumaanishi kuwa mtu ana kinga dhidi ya maambukizi mapya.

“Wakati huu hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa watu ambao wamepona kutokana na Covid-19 wana kingamwili (anti bodies) ambayo itawazuia kupata maambukizi kwa mara nyingine,” WHO ilisema kwenye taarifa wakati ambapo idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo imevuka wahanga 200,000.

Onyo hilo la WHO linajiri wakati ambapo baadhi ya mataifa yanatumia idadi ya watu waliopona kama sababu ya kuweka kando na amri za kuwazuia watu kutotoka nje na kuruhusu kufunguliwa kwa biashara.

WHO inawaonya watu waliopona kwamba wanafaa kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara za afya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona kama vile; kuvalia maski, kutotangana na kudumisha usafi kila mara.

Katika mataifa mengi, kuna wasiwasi wa kutokea kwa awamu ya pili ya maambukizi baada ya amri za kutotoka nje kulegezwa.

Kwa mfano katika taifa la Iran lililoathirika zaidi ya ugonjwa wa Covid-19, maafisa wa afya Jumapili walielezea hofu ya kuzuka kwa maambukizi mapya. Na jumla ya watu wagonjwa 76 wa covid-19 walifariki Jumapili, na kufikisha 5,650 idadi ya waliofariki nchini Iran kufikia Jumapili kutokana na ugonjwa huo hatari.

Iran ilikuwa imearuhusu kufungiliwa kwa biashara zilizokuwa zimefungwa ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Hata hivyo, Alireza Zali, ambaye ni mshirikishi wa afya katika jiji kuu, Tehran, alipinga kufunguliwa kwa biashara akisema, hatua hiyo inaweza kusababisha awamu mpya maambukizi ya virusi vya corona.

You can share this post!

Watu 18 wakamatwa jijini Nairobi wakiwa uchi

Serikali yatangaza kanuni mpya za kufungua mikahawa

adminleo