Iran yaionya vikali Amerika
NA MASHIRIKA
RAIS wa Iran Hassan Rouhani alisema Jumanne kwamba amani na nchi yake itakuwa “mama wa amani yote” na vita na Iran vitakuwa “mama wa vita vyote.”
“Usalama kwa usalama, amani kwa amani. Huwezi kudhuru usalama wetu na utarajie usalama kwako.
“Amani kwa amani na mafuta kwa mafuta,’” alisema Rouhani alipozuru Wizara ya Masuala ya Kigeni katika mkutano na Waziri Zarif, aliyewekewa vikwazo na Amerika mnamo Julai 31, manaibu wake na maafisa wa wizara hiyo.
Matamshi yake yalilenga utawala wa Rais Donald Trump ambao umeanzisha vita vya kiuchumi dhidi ya Iran kwa kupiga marufuku bidhaa za mafuta zinazoagizwa kutoka Iran na kutuma ndege aina ya B-52 ulipuaji bomu, ndege za kivita aina ya F-22 na mamia ya vikosi katika eneo la ukanda wa Gulf katika kisingizio kwamba unataka kuzuia uwezekano wa shambulizi lolote kutoka Iran
Imetafsiriwa na Mary Wangari