Israel yaua wana 3 wa kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh
UKANDA WA GAZA
NA MASHIRIKA
WANA watatu wa kiongozi Mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh waliuawa katika shambulizi la anga lililotekelezwa na Israel katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumatano.
Israel ilithibitisha shambulizi hilo, likitaja ndugu hao kuwa wanachama wa mrengo wa kijeshi wa Hamas.
Watatu hao; Hazem, Amir na Mohammad waliuawa wakati gari walilokuwa wakiendesha lilipolipuliwa kwa bomu katika kambi ya Al-Shati ya Gaza, Hamas.
Pia, wajukuu wanne wa Haniyeh, wasichana watatu na mvulana mmoja, waliuawa kwenye shambulio hilo.
Bw Haniyeh, 61, baba wa watoto 13, alithibitisha taarifa hiyo akitaja kuwa ni ulipizaji kisasi.
Soma pia: Huenda mnichukie lakini lazima tuvamie Rafah, Netanyahu asema
Kulingana na jamaa wa familia hiyo, alisema saba hao (wanawe watatu na wajukuu wanne) waliuawa walipokuwa wakifanya ziara za kifamilia wakati wa sikukuu ya Idd ul-Fitr ya Waislamu huko Shati, kwenye kambi ya wakimbizi ya Gaza.
Siku ya Jumanne, Hamas ilisema inachunguza pendekezo la Israel la kusitisha mapigano katika vita vya Gaza vilivyodumu kwa zaidi ya miezi sita lakini halikuwa na mvuto na halikukidhi matakwa yoyote ya Wapalestina.
“Madai yetu yako wazi. Hatutaweka makubaliano na wao. Adui atakuwa mdanganyifu akidhani kuwalenga wanangu, katika kilele cha mazungumzo. Kabla ya harakati hiyo ya kupeleka majibu yake, tutaisukuma Hamas kubadili msimamo wake,” aliongeza Bw Haniyeh.
Katika kipindi cha miezi sita ya vita vya mashambulizi ya anga na ardhi ambayo yameharibu Gaza, Hamas inataka kusitishwa kwa operesheni za kijeshi za Israeli na kujiondoa katika eneo hilo na kuruhusu wakimbizi wa Kipalestina kurejea makwao.
Mnamo 2017, Bw Haniyeh aliteuliwa kuchukua nafasi ya ngazi ya juu kwenye kazi ya jeshi. Alihamia nchi ya Uturuki na mji mkuu wa Qatar Doha anapoishi kwa sasa, ili kuepuka vikwazo vya kusafiri vilivyowekwa na Israel. Hali hiyo ilimwezesha kuwa msuluhishi katika mazungumzo ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano au kuwasiliana na mshirika mkuu wa Hamas ambaye ni Iran.
Israel inachukulia uongozi wa Hamas kuwa wa kigaidi, ikimtuhumu Haniyeh na viongozi wengine kwa kuendelea miungano ya ugaidi huko Hamas.
Lakini haifahamiki jinsi Bw Haniyeh alijua kuhusu shambulio la Oktoba 7 kuvuka mpaka dhidi ya Israeli na wanamgambo wa Gaza.
Mpango wa mashambulizi, uliotayarishwa na baraza la kijeshi la Hamas huko Gaza, ulikuwa siri yenye ulinzi mkali kiasi kwamba baadhi ya maafisa nje ya nchi hiyo walionekana kushangazwa.