Kimataifa

Mkubali masharti au muondoke, Magufuli aambia Wachina

December 4th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

NA AFP

JUHUDI za China za Ujenzi wa Barabara Majini zilipata pigo baada ya serikali ya Tanzania kukataa kulegeza msimamo wake katika majadiliano yaliyokwama kuhusu ujenzi wa bandari ambayo ingekuwa kubwa zaidi na yenye kina kirefu Afrika.

Maafikiano kuhusu mradi huo ulioafikiwa kwa mara ya kwanza 2013, yamesalia suala tata linalozua mvutano kati ya Rais wa Tanzania John Magufuli na kampuni ya China Merchants Holdings, shirika la Uchina lililopangiwa kujenga bandari hiyo na miundomsingi husika.

Tanzania ilifutilia mbali mradi huo hadi kwa muda usiojulikana mnamo Juni na ikakosa kuonyesha ishara zozote za kubadili nia katika mkutano uliondaliwa Oktoba.

Badala yake, serikali ya Tanzania ilitoa makataa thabiti kwa kampuni hiyo ya Uchina: mkubali masharti yetu au muondoke.

Ingawa Uchina na viwanda vya Uchina vingali wawekezaji wakuu katika miundomsingi ya Afrika hasa bandari, mvutano kuhusu bandari ya Bagamoyo unadhihirisha kuwa viongozi wa Afrika wanageuka kuwa wanaodai miradi inayofadhiliwa na Uchina kuwiana na mahitaji ya maendeleo Afrika au angalau maslahi ya kisiasa Afrika.

Mgogoro huu pia unaibua maswali kuhusu mtindo wa biashara wa Uchina na kile ambacho maafisa wa Amerika wanataja kama “mtego wa deni kidiplomasia’ wa Uchina.

Ingawa haya ni masuala yanayopaswa kuangaziwa, suala tata kwa viongozi wa Afrika ni kuongeza shinikizo kwa miradi hii ya miundomsingi kuwa na matokeo nchini mwao.