Pompeo ajikuna kichwa kupatanisha Israeli na Palestina
Na MASHIRIKA
TEL AVIV, ISRAEL
WAZIRI wa Mambo ya Kigeni wa Amerika Mike Pompeo alifika nchini Israel Jumapili katika kipindi cha kuzorota zaidi kwa uhusiano baina ya Waisreali na Wapalestina, lakini hakufanikiwa kukutana na mwakilishi yeyote wa Palestina huku akiwataja hadharani mara moja tu.
Kwa miongo mingi, mabalozi wa Amerika wamekuwa wakipatanisha pande hizo mbili, huku wakikutana ana kwa ana na wawakilishi wa Palestina katika ziara kama ya Bw Pompeo.
Wakati uhusiano wa pande hizo mbili ulionekan akufikia hatuahatri, Amerika ilijitolea kutoa upatanisho.
Lakini hana yeyote katika Wizara ya Mambo ya Kigeni aliwapigia simu viongozi wa Palestina kuuliza kuhusu kukutana na Bw Pompeo, kwa kuwa tayari walijua haingekubalika.
Wakionekana kukerwa sana na uamuzi wa Rais Donald Trump wa kuitangaza Jerusalem kama jiji kuu la Israel, na kuhamisha afisi zao za ubalozi kutoka Tel Aviv, viongozi wa Palestina wamekata mawasiliano ya kisiasa baina yao na utawala wa Trump.
Wanasema kuwa Amerika haiwezi kuaminika tena katika mchakato wa kuleta amani baina ya pande hizo mbili.
“Hakuna jambo la kujadili,” akasema Xavier Abu Eid, afisa mkuu wa Idara ya Upatanisho la Shirika la Ukombozi la Palestina.