• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Rais mpya wa Tunisia aapishwa

Rais mpya wa Tunisia aapishwa

Na MASHIRIKA

TUNIS, TUNISIA

RAIS mpya wa Tunisia Kais Saied ameapishwa rasmi kwenye kikao cha bunge la taifa hilo.

Saied, 61 ambaye pia ni msomi mhafidhina alichukua mamlaka ya kuongoza taifa hilo baada ya kushinda katika duru ya pili ya uchaguzi ulioandaliwa majuma mawili yaliyopita.

Alishinda kwa asilimia 72.71 dhidi ya mpinzani wake Nabil Karoui, tajiri mmiliki wa vyombo vya habari ambaye alijizolea asilimia 55.

Akihutubu baada ya kulishwa kiapo, Rais Saied ameahidi kuzingatia utekelezwaji wa demokrasia na kutimiza ahadi alizotoa kwa raia wakati wa kampeni.

Wadadisi wamesema kwamba Rais huyo huenda akasaidia kurejesha taifa hilo katika hali yake ya udhabiti kama zamani kutokana na sera zake ambazo zinaangazia masuala ya kijamii na kupendekeza adhabu kali kwa mafisadi.

Karoui, 56 ambaye alikuwa akizuiliwa kwa kosa la utakatishaji wa fedha kabla ya kuachiliwa Agosti 23 alikubali kushindwa licha ya kufanya kampeni kali na kukutana na watu kutoka maeneo mbalimbali.

You can share this post!

SEKTA YA ELIMU: Mageuzi yanahitajika katika elimu ya vyuo...

SHANGAZI AKUJIBU: Mke ananikosesha amani kwa kuwachukia...

adminleo