Rais Trump akutana na mwenzake wa Korea Kusini Lee Jae Myung
RAIS wa Amerika, Donald Trump Jumatano alikutana na mwenzake wa Korea Kusini Lee Jae Myung katika mji wa kihistoria wa Gyeongju.
Ziara ya Trump nchini Korea Kusini inafanyika wakati Korea Kaskazini ikisema kuwa imerusha makombora ya masafa marefu katika bahari yake ya magharibi, ikiwa ni onyesho lake jingine la kuongezeka kwa uwezo wake wa kijeshi.
Akizungumza kabla ya kukutana na Trump, Rais Myung wa Korea Kusini alionya kuhusu ongezeko la sera za kiuchumi duniani ambapo serikali zinalinda viwanda vya ndani dhidi ya ushindani wa nje kwa kuweka vikwazo vya kibiashara ikiwemo ushuru kwa bidhaa za nje.
Kabla ya kuelekea Korea Kusini, Rais Trump alizuru Japan na kufikia mkataba wa uwekezaji wa mabilioni.