Rais wa zamani wa Burundi kubambwa kuhusu mauaji
Na MASHIRIKA
BUJUMBURA, Burundi
TAIFA la Burundi limetoa ilani ya kukamatwa kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Pierre Buyoya na maafisa wakuu 16 wa zamani katika serikali yake kwa kuhusika katika mauaji ya matangulizi wake, Buyoya, Melchior Ndadaye.
“Matokeo ya uchunguzi yanaonyesha kuwa watu hawa walihusika katika uhalifu huu…. mipango yake na hata utekelezaji,” Mkuu wa Sheria Sylvester Nyandwi aliwaambia wanahabari Ijumaa jioni.
Ndadaye ndio alikuwa kiongozi wa kwanza kutoka kabila wa Wahutu aliyechaguliwa kidemokrasia.
Wengine ambao Burundi inataka wakamatwe ni pamoja na maafisa 11 wakuu wa kijeshi na raia watano ambao walikuwa wandani wa karibu wa Buyoya.
Burundi inataka mataifa mbalimbali ambako watu hawa wanaishi kama wakimbizi yawarejeshe nchini humo ikisema: “Ni muhimu kwa watu hawa kuhojiwa kuhusiana na michango yao” katika mauaji hayo.
Wakati huu Boyoya ni balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Mali na kiongoi anayeheshimika barani Afrika na ng’ambo.
Kiongozi huyo, ambaye ni Mtutsi, aliingia mamlakani mnamo 1987 baada ya kusaidiwa na wanajeshi.
Aliondoka mamlakani mnamo 1993 Ndadaye alipochaguliwa. Lakini Ndadaye aliuawa miezi minne katika mapinduzi yaliyoongozwa na wanajeshi wa kabila la Tutsi.