Wabunge wawili wa Uingereza wazuiwa kuingia Uingereza
LONDON, Uingereza
WABUNGE wawili wa Uingereza walizuiwa kuingia nchini Israel walipokuwa wakielekea eneo la West Bank.
Abtisam Mohamed, ambaye ni Mbunge wa Sheffield na mwenzake Yaun Yang ambaye ni Mbunge wa Earley and Woodley walikuwa wakisafiri kwa ndege kutoka London ili kushuhudia hali katika himaya hiyo ya Palestina inayotawaliwa na Israel.
Lakini utawala wa Israel uliwazuia kuingia nchini humo ndiposa waweze kufika West Bank.
Idara ya Uhamiaji ilisema wabunge hao wa chama cha Labour walizuiwa kuingia kwa sababu “walilenga kueneza chuki dhidi ya Israel, raia wake na maafisa wa Idara ya Uhamiaji.”
Idara hiyo ilisema Waziri wa Masuala ya Ndani wa Israel ndiye aliamuru Mbw Mohamed na Yang wazuiliwe kwa sababu walitaka kunakili maelezo kuhusu shughuli za wanajeshi wa nchi hiyo katika West Bank.
Imeandaliwa na Charles Wasonga