• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Watu tisa waliokamatwa kwa kumzomea mke wa rais waachiliwa

Watu tisa waliokamatwa kwa kumzomea mke wa rais waachiliwa

NA MASHIRIKA

WANAWAKE tisa waliokamatwa nchini Zimbabwe kwa madai ya kumzomea mke wa rais Auxillia Mnangagwa wameondolewa mashtaka, vyombo vya habari vimeripoti.

Mashtaka hayo yaliondolewa kufuatia agizo la Bi Mnangagwa, ripoti hizo jzikasema zikimnukuu msemaji wa rais George Charamba jana.
“Mama wa taifa na kamishna wa polisi wamekubaliana kwamba maafisa wahusika walichukua hatua ambayo haikuhitajika,” Bw Charamba akasema.

Ilidaiwa wanawake hao, wenye umri wa kati ya miaka 19 na 49, walimzomea Bi Mnangagwa baada ya kukosa zawadi ya chakula na mguo alizokuwa akiwagawa katika mkoa wa Manicaland Ijumaa wiki jana.

“Waendesha mashtaka walisema kuwa wanawake hao waliokuwa wameketi chini alinyanyuka na kuanza kumzomea mke huyo wa Rais Emmerson Mnangagwa alipokuwa akitoa hotuba yake kuonyesha kuridhishwa kwao baada ya kukosa zawadi,” Mawakili wa Zimbabwe kuhusu Haki za Kibinadamu (ZHLR) waliowawakilisha wanawake walisema kortini.

  • Tags

You can share this post!

Vijana waliotaabika bila kazi walivyojijengea viota vya...

Demu azua kisanga akitimua jombi aliyekwamilia kwake

T L