Habari

Ndege ya KQ kwenda Dar es Salaam yaagizwa kurudi Nairobi dakika 25 baada ya kupaa

Na FATUMA BARIKI April 27th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

NDEGE ya KQ kutoka JKIA kwenda Dar es Salaam, Tanzania imeagizwa kurejea Nairobi dakika 25 baada ya kupaa kufuatia hofu ya kuvuja kwa kemikali hatari kwenye eneo la mizigo, wasafiri katika ndege hiyo wameripoti.

Kulingana na ripoti hizo, ndege hiyo KQ484 tayari ilikuwa hewani wakati agizo lilipotumwa kwamba ipige kona na kurejea Nairobi mara moja huku abiria wakiambiwa kuna hatari kwamba bakteria aina ya Tuberclosis Bacilli huenda ilivuja kutoka kwa eneo la mizigo wakati wa safari ya awali.

Abiria wameambiwa wasiondoke na maafisa wa afya wameingia kwenye ndege hiyo kuchukua maelezo yao. Eneo la mizigo limepuliziwa dawa na kufikia wakati wa kuandika taarifa hii, bado ndege hiyo haikuwa imeruhusiwa kuendelea na safari huku abiria wakianza kuzusha.