Vipusa watoroka kidume mwenye nguvu za kukausha ‘bahari ya mahaba’
SHANZU, MOMBASA
JAMAA mmoja kutoka mtaani hapa amezua hisia mseto baada ya kudai kuwa wanawake wengi wamekuwa wakimkimbia kwa sababu ya “mbio zake kali” chumbani.
Kalameni huyo alisema licha ya kuwa na mapenzi ya kweli na nia njema ya kudumu katika mahusiano, wanawake wanaojaribu kuwa naye huishia kumpa kisogo kwa madai kuwa hawajali chumbani.
“Kila nikijaribu kuwa na mahusiano ya muda mrefu, huishia kuvunjika. Wanasema mbio zangu chumbani ni za ajabu – sijui ni kosa langu kuwa na nguvu,” alilalamika kwa masikitiko katika ukurasa mmoja mtandaoni.
“Kila mtu ana mahitaji tofauti. Si mbio wala kasi inayojenga uhusiano, ni ustadi na kujali mtu wako,” alisema demu mmoja.
Jamaa alialika demu yeyote aliye tayari kuvumilia miondoko yake amtafute.