Wandayi ashutumu Kalonzo, Wamalwa kuhusu NADCO
WAZIRI wa Kawi Opiyo Wandayi amewataka viongozi wa upinzani wawe waaminifu wanapowasilisha sera zao.
Bw Wandayi hasa alichemkia matamshi ya Kinara wa Upinzani Kalonzo Musyoka na Kiongozi wa DAP- Kenya Eugene Wamalwa waliodai kuwa Ripoti ya Jopokazi la Maridhiano (NADCO) haijatekelezwa kikamilifu.
Wawili hao waliyatoa matamshi hayo wakati wa mazishi ya Beryl Odinga, dadake, Waziri Mkuu wa zamani marehemu Raila Odinga, eneobunge la Bondo.
Bw Wandayi alisema kuwa ni kupitia ripoti ya NADCO ndipo kwa sasa kuna Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC).
Aidha, Waziri huyo alimshutumu Bw Wamalwa kwa kuzungumzia ripoti ya jopokazi la maridhiano ilihali alikataa kuitia saini.