Kimbunga hatari chapiga Hong Kong
RAGASA, kimbunga chenye nguvu zaidi duniani umewaacha mamilioni ya watu kusini mwa China bila makazi na kuua watu 14 Taiwan.
Kimbunga hichi pia kimeshambulia Hong Kong kwa upepo mkali na mvua kubwa.
Takriban watu 129 hawajulikani waliko katika maeneo ya mashariki ya Taiwan ya Hualien, baada ya ziwa kufurika na kuzamisha mji mmoja katika eneo hilo.
Wakazi wengi katika mji wa kitalii wa Guangfu walilalamika kuwa hakukuwa na onyo la kutosha kutoka kwa mamlaka ya Taiwan, ambao wamezoea kuwahamisha watu kutoka katika maeneo hatari kwa haraka kwenye kisiwa hicho ambacho mara kwa mara hukumbwa na vimbunga.
Mvua ilipogonga Taiwan, Hong Kong ilikabiliana na mawimbi makubwa ambayo yalipiga maeneo ya ufuo wa mashariki na kusini jambo lililofanya barabara na makazi kuzama.
Katika hoteli ya Fullerton iliyoko kusini mwa kisiwa hicho, video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha maji yakipita kwenye milango na madirisha.
Mamlaka ya majini China ilitoa onyo la juu zaidi la mawimbi ‘nyekundu’ kwa mara ya kwanza mwaka huu, ikitabiri mawimbi ya dhoruba ya hadi mita 2.8 (futi 9) katika sehemu za mkoa wa Guangdong, wakati Ragasa ikishambulia Delta ya Mto Pearl yenye wakazi wengi.
Ragasa ilijitokeza Magharibi mwa Pasifiki wiki iliyopita na kikichochewa na joto na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kimbunga hicho cha kitropiki kiliimarika kwa kasi na kuwa kimbunga kikubwa siku ya Jumatatu chenye upepo unaozidi 260 kph (162 mph).
Tangu wakati huo, kimbunga hicho kimedhoofika na kufikia kiwango cha 3, ambacho bado kinaweza kuangusha miti na nyaya za umeme, kuvunja madirisha na kuharibu majengo.
‘Mamlaka ilijifunza kutoka kwa Hato na Mangkhut, ambayo yote yalisababisha uharibifu wa mabilioni mnamo 2017 na 2018,’ Chim Lee, mtaalamu mkuu wa nishati na mabadiliko ya hali ya hewa katika Kitengo cha Ujasusi cha Economist alisema.
‘Delta ya Mto Pearl ni mojawapo ya maeneo ambayo yameundwa vyema zaidi kukabiliana na vimbunga, kwa hivyo hatutarajii usumbufu mkubwa. Mabadiliko moja mwaka huu ni kwamba soko la hisa la Hong Kong limesalia wazi wakati wa vimbunga – ishara ya jinsi miundombinu imekuwa thabiti,’ aliongeza.