NASAHA ZA RAMADHAN: Chakula cha daku humpa nguvu mfungaji na humchangamsha
Na KHAMIS MOHAMED
WENGI wetu tunaofunga tunaona kula daku ni jambo dogo tu ilhali ni jambo lililokokotezwa sana na Uislamu kama tunavyojifunza katika Qur’an na Hadithi za Mtume Muhammad (Rehma na aman?z?mf?k?e): “…..Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku…..” (Qur’an: 2:187).
Mtume Muhammad (S.A.W) amesisitiza sana kula daku. Tuone hadithi moja ifuatayo: “Kuleni daku, kwani ipo baraka katika kula daku. Na tofauti ya fadhila ya funga zetu sisi Waislamu na Ahlul Kitabu (Wayahudi na Wakristo) ni huko kula daku.
Daku au “as-suhuur” ni chakula kinacholiwa wakati wa ‘al as-haar’ ambao ni wakati wa robo ya mwisho ya usiku. Daku ni chakula baada ya mtu kulala kisha akaamka kwa ajili hiyo. Na lengo la daku ni kumfanya mfungaji kupata nguvu mchana wa Ramadhani.
Utaratibu huu wa kula daku kwa Waislamu umeamrishwa na kuhimizwa na Mtume (S.A.W) aliposema “Ni juu yenu kula daku, kwani ni chakula kilichobarikiwa” (An Nasaaiy kwa sanad Jayyid)
Chakula cha daku humpa nguvu mfungaji, na kumfanya awe mchangamfu, na mwepesi katika funga yake.
Baraka ya daku haipatikani kwa kiwango kingi cha chakula au kichache, bali hupatikana hata kwa funda la maji. Imepokewa na Abi Said Al-khudriy (r.a), kuwa:“Daku ni baraka, msiiache walau kwa kunywa mmoja wenu funda ya maji, kwani MwenyeziMungu na Malaika wake huwarehemu wanaokula daku”. (Imepokewa na Ahmad).
Nusu ya usiku
Daku huliwa kwenye nusu ya usiku mpaka karibu ya mapambazuko ya alfajiri, na ni vyema kula wakati wa mwisho.
Kama ilivyopokelewa na Zaid bin Thabit (r.a) akisema: “Tulikula daku pamoja naMtume (S.A.W), kisha tukaenda kuswali. Nikasema:kulikuwa na (tofauti ya) muda gani baina yamawili hayo? Akasema: Aya khamsini”. [Im-epokewa na Bukhari na Muslim].
Na kutoka kwa Amri bin Maymun aliele-za: “Walikuwa Swahaba wa Mtume (rehmana amani ya Allah iwe juu yake), wanaharakisha sana kufuturu, na kuchelewesha sana kula daku”. [Imepokewa na Bayhaqiy kwasanad sahih].
Hata kama mtu atatia shaka ya kuchomoza kwa alfajiri, sharia inamtaka ale, na anywe,mpaka awe na yakini ya kuchomoza kwa alfajiri ya kweli.