Shangazi Akujibu
SHAGAZI AKUJIBU: Ananisubiri na vyombo kila nikimtembelea
Mwanamke akifanya kazi za nyumbani. Picha| Maktaba.
SWALI: Mwanaume ninayempenda hukula na kuacha vyombo mezani bila kuosha. Chumba hakifagiliwi hadi mimi nirudi. Huwa namtembelea kila wikendi na nikifika nyumba ina harufu baya. Nimechoka kubebwa kama mbochi. Nipe ushauri.
Jibu: Zungumzeni umwambie unachohisi. Kando na hayo, anafaa kufahamu kuwa wewe si mfanyakazi wake bali ni mpenzi wake.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO