
Wanandoa waliozama kwenye mapenzi. PICHA|HISANI
Swali: SHIKAMOO shangazi. Mume wangu ana tabia ya kunichunguza kwa kuingiza vidole kwenye sehemu zangu za siri na kunusa kabla ya kushiriki tendo la ndoa.
Nikimuuliza, anadai kuwa anahakikisha sitembei nje ya ndoa. Tabia hii inanidhalilisha na kunikera sana. Naomba ushauri.
Jawabu: Tabia ya mume wako inaashiria ukosefu wa imani na heshima katika ndoa yenu. Zungumza naye kwa utulivu, ukimweleza jinsi unavyohisi.
Ikiwa hatabadilika mshirikishe mshauri wa ndoa au mtaalamu wa afya ya akili. Haki yako ya heshima na faragha inapaswa kulindwa kila wakati.