Habari Mseto

Mgomo wa maafisa wa afya wachacha Homa Bay

August 10th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Shughuli za maswala ya afya Homa Bay zimelemazwa na mgomo unaoendelea wa maafisa wa afya.

Maafisa hao wanalalamikia ukosefu wa vifaa vya kujikinga huku wakisema kwamba wako kwenye hatari ya kupata virusi vya corona wakiwa kazini.

Katika mazishi ya mwenazo Bi Marianne Awuor aliyefariki kutokana na virusi vya corona wiki iliyopita, swala la jinsi kaunti hiyo imejitayarisha kupambana na virusi vya corona lilizuka.

Bi Awuor alizikwa jumaa asubuhi kwenye kijij cha Nyandonge, Kasipul.

Iliibuka kwamba kulikuwa na kuchelewa kwa huduma ya kwanza alipolazwa baada ya kuonyesha virusi vya corona,

Familia yake ilisema kwamba iliwachukua saa tano kabla ya ambulensi ya msalaba mwekundu kuwasili kutoka Homabay hadi Oyugis kumchukua muuguzi huyo, aliyekua mjamzito wakati ambapo hali yake ya afya iliendelea kudhoofika..

Alikuwa apelekwe kwenye hospitali ya rufaa ya Kisii ambayo inaaminika kuwa na vitanda cha wagonjwa mahututi.

Hospitali ya Rachuonyo ilikana madai hayo.

Maafisa wa afya wa Homabay waligoma wiki iliyopita kudai mshahara wa Juni na Julai pamoja na vifaa vya kujikinga kutokana na virusi vya corona.