Michezo

GSU ya Kenya yapata kundi rahisi kwenye droo ya voliboli Cairo

March 26th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na GEOFFREY ANENE

DROO ya mashindano ya voliboli ya wanaume ya Klabu Bingwa Afrika imefanywa jijini Cairo, Misri, Jumatatu, huku General Service Unit (GSU) ikitiwa katika Kundi D, ambalo linaonekana rahisi.

Wawakilishi wengine wa Kenya, Prisons, wamekutanishwa na mabingwa mara 12 na wenyeji Al Ahly, ambao wanatetea taji, katika Kundi A.

Miamba wa Kenya, GSU, ambao walishinda medali ya shaba mwaka 2005, watalimana na Port (Cameroon), Olympique (Algeria), Kampala (Uganda), GSU (Kenya), Wolaitta (Ethiopia) na mabingwa wa mwaka 2016 Tala’ea El-Gaish (Misri).

Prisons, ambao walinyakua medali ya fedha mwaka 2011, wako kundi moja na Ahly (Misri), Prisons (Kenya), Police (Ivory Coast), Espoir (DR Congo), Nemo Stars (Uganda), Redskin (Lesotho).

Klabu za Kenya hazijawahi kushinda taji.

Mechi zinatarajiwa kuanza Machi 27 na kukamilika Aprili 5, 2018.

 

Makundi:

A – Ahly (Misri), Prisons (Kenya), Police (Ivory Coast), Espoir (DR Congo), Nemo Stars (Uganda), Redskin (Lesotho);

B – Al Swehly (Libya), Finances (Benin), Swim Blue Pal (Ushelisheli), DGSP (Congo Brazzaville), Aviation (Misri), Bafia (Cameroon);

C – FAP (Cameroon), AS Police (Benin), Ahly Benghazi (Libya), University of Zimbabwe (Zimbabwe), Smouha (Misri), Mwangaza (DR Congo)

D – Port (Cameroon), Olympique (Algeria), Kampala (Uganda), GSU (Kenya), Wolaitta (Ethiopia), Tala’ea El-Gaish(Misri).