• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
Diamond League 2022 kuanza Mei 13

Diamond League 2022 kuanza Mei 13

Na GEOFFREY ANENE

Shirikisho la Riadha Duniani limetangaza ratiba ya mbio za riadha za Diamond League mwaka 2022.

Mshikilizi wa rekodi ya Afrika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala anatarajiwa kuanza kushiriki mashindano hayo mwaka ujao. Duru ya Doha nchini Qatar itakuwa ya kwanza mnamo Mei 13 ikifuatiwa na Birmingham/London nchini Uingereza (Mei 21), Eugene nchini Amerika (Mei 28), Rabat nchini Morocco (Juni 5) na Roma nchini Italia (Juni 9).

Msimu huo utafika katikati mnamo Juni 16 wakati Olso nchini Norway itaandaa duru ya saba ambayo itafuatiwa na Paris nchini Ufaransa (Juni 18), Stockholm nchini Uswidi (Juni 30), Shanghai, Uchina (Juli 30), Uchina (Agosti 6) na Monaco (Agosti 10). Duru za Lausanne, Uswisi (Agosti 26), Brussels, Ubelgiji (Septemba 2) na Zurich, Uswisi (Septemba 7-8) zitakamilisha msimu huo.

Wakenya Faith Chepng’etich (mita 1500), Norah Jeruto (mita 3,000 kuruka viunzi na maji), Benjamin Kigen (mita 3,000 kuruka viunzi na maji), Timothy Cheruiyot (mita 1,500) na Emmanuel Korir (mita 800) walishinda mataji katika vitengo hivyo vyao msimu uliopita.

You can share this post!

Ruto: Rais hatakuwa ameafikia ajenda zake atakapostaafu

Sonko azimwa kurusha video za Kananu

T L