• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 7:50 AM
Khaniri awarai Waluhya wamuunge mkono Raila

Khaniri awarai Waluhya wamuunge mkono Raila

NA DERICK LUVEGA

SENETA wa Vihiga George Khaniri ameiomba jamii ya Waluhya imuunge mkono kwa mara nyingine Kinara wa ODM Raila Odinga katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Bw Khaniri amesema kuwa ni kupitia Urais wa Bw Odinga ambapo jamii hiyo nayo itakuwa na nafasi kuingia katika ikulu mwaka 2027.

Mwanasiasa huyo alisema Waluhya ndio watapoteza zaidi iwapo watashawishika kuunga mkono mrengo wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Naibu Rais Dkt William Ruto, kinara wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetang’ula.

Bw Khaniri ambaye analenga kiti cha ugavana wa Vihiga kupitia United Democratic Party (UDP), alisema kuwa mwaniaji Mluhya yupo pazuri kutwaa kiti cha urais iwapo watamuunga mkono Bw Odinga. UDP inaongozwa na mbunge wa zamani wa Lugari Cyrus Jirongo.

Bw Khaniri alikuwa akizungumza katika eneobunge la Hamisi ambapo aliahidi kuwa akichaguliwa gavana, ataongoza kwa muhula mmoja kisha kuwania urais 2027.

“Sisi katika UDP tunaunga mkono Raila Odinga kwa sababu ndiye anafaa zaidi. Kwa kuwa urais utakuwa karibu hapa Ziwa Viktoria, itakuwa rahisi kutua hapa Magharibi baada ya Raila kumaliza hatamu yake,” akasema Bw Khaniri.

Alikariri kuwa atawania Urais 2027 na ana imani ataungwa mkono na Bw Odinga.

Aliwakemea Mabw Mudavadi na Wetang’ula akisema wamesaliti jamii hiyo kwa kumuunga Dkt Ruto ambaye alimtaja kama kiini cha umaskini ambao Wakenya wanapitia.

You can share this post!

Arsenal kuzidisha mshahara wa Saka mara nne

Ida aahidi kuinua maisha ya wanawake vijijini Raila akiwa...

T L