• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Bomoabomoa sasa zamfikia pia Askofu Margaret Wanjiru

Bomoabomoa sasa zamfikia pia Askofu Margaret Wanjiru

NA NYABOGA KIAGE

KANISA la Askofu Margaret Wanjiru wa Jesus is Alive Ministries limebomolewa kufuatia mzozo wa umiliki wa ardhi kati ya kanisa hilo na Shirika la Reli nchini (KRC).

Mnamo Jumatano, vijana walianza kulibomoa kanisa hilo kwa mabavu huku wakidai kuwa walikuwa wametumwa na KRC.

Bi Wanjiru ambaye pia ni mwanasiasa anayehusishwa na chama cha Rais William Ruto cha United Democratic Alliance (UDA) alikemea hatua hiyo akisema haifai.

“Si haki watu kuja hapa na kuanza kulibomoa kanisa langu,” alisema Bi Wanjiru.

Alipokuwa akihutubia wanahabari, Bi Wanjiru alisema kwamba vijana walibomoa ukuta unaotenganisha kanisa hilo na Shirika la Reli nchini.

Vijana hao walilenga ukuta ambao walidai kuwa si mali ya Bi Wanjiru.

“Kati ya vijana hao, wengine walisema wanatoka Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS), wengine wanadai kutoka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI) na wengine kutoka kwa polisi,” alilalamika.

Bi Wanjiru anasema kuwa serikali ilihusika katika kashfa hiyo.

“Kwa hivyo bila shaka serikali inahusika, na inasikitisha kwamba hii ndiyo serikali ambayo tuliipigia kura,” akaongeza Bi Wanjiru.

  • Tags

You can share this post!

Mcheshi Muthee Kiengei sasa kutawazwa kuwa Askofu

Waziri Mkuu wa Haiti ‘ahepea’ Puerto Rico

T L