• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Msako dhidi ya makahaba wanaomezea mate hela za wakulima waanza

Msako dhidi ya makahaba wanaomezea mate hela za wakulima waanza

NA TITUS OMINDE

POLISI wa Kaunti ya Uasin Gishu wameimarisha msako dhidi ya makahaba mjini humo kwa lengo la kulinda wakulima ambao wanapokea pesa za malipo ya mahindi.

Msako huo uliimarishwa kuanzia wiki iliyopita punde tu baada ya serikali kuanza kulipa wakulima ambao waliwasilisha zao la mahindi katika mabohari ya Bodi ya Kitaifa ya Mazao na Nafaka (NCPB).

Polisi walisema msako huo ulichochewa na ongezeko la idadi ya makahaba ambao wanadaiwa kulenga wakulima wazee hasa wale wa kutoka maeneo ya mashambani.

“Hii biashara ni haramu. Hatutaruhusu watu wavivu ambao hawataki kufanya kazi halali waendelee kutumia ukahaba kupora wakulima mali yao ambayo wameipata kwa jasho,” alisema mmoja wa maafisa wa polisi anayeongoza oparesheni hiyo na ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Makahaba wanaolengwa walisema uchumi wao umezorota kama wa Wakenya wengine na kile wanachotaka ni kujitafutia riziki.

“Tunahangaishwa mchana na usiku, ajabu ni kwamba tukifika kortini makosa ambayo tunashtakiwa nayo huwa tofauti,” alisema mmoja wa makahaba hao ambaye alitaka jina lake libanwe.

Mwaka uliopita wazee kadhaa ambao ni wakulima walidai kuporwa zaidi ya Sh500,000 kwa jumla na wanawake ambao wanafahamika kuwa makahaba katika madanguro ya Eldoret.

You can share this post!

Mtaala mpya uko sambamba, haujakwama – KICD

Wahisani waagizwa kutii kanuni za KCPE wakitoa mlo

adminleo