Maadhimisho ya Idd-Ul-Fitr
NA SAMMY WAWERU
JAMII ya Dini ya Kiislamu Jumatano, Aprili 10, 2024 walikongamana katika maeneo mbalimbali ya kuabudu kuadhimisha Sikukuu ya Id-Ul-Fitr.
Sikukuu ya Id-Ul-Fitr inaashiria mwisho wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mwezi huo ni wa tisa katika kalenda ya Kiislamu.
Sherehe za Id-Ul-Fitr huanza kwa maombi maalum yanayojulikana kama; Eid, yanayofanyika alfajiri baada ya mwezi kuonekana.
Baadaye, hushiriki karamu ya mlo na pia hualika umma kusherehekea.
Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof Kithure Kindiki kupitia taarifa alitangaza jana, Jumanne, Aprili 9, 2024 kwamba leo – Jumatano itakuwa Sikukuu kwa minajili ya maadhimisho ya Id-Ul-Fitr.
Zifuatazo ni picha za Waislamu kutoka maeneo tofauti nchini wakisali.