Enterprise Cup: Kabras wafinya KCB na kuhifadhi taji
Na GEOFFREY ANENE
KABRAS Sugar kutoka kaunti ya Kakamega sasa wako ligi moja na Nondescripts, Eldoret na Impala katika kushinda mataji manne ya mashindano ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya Kombe la Enterprise.
Hiyo ni baada ya Kabras kuzoa taji la nne kwa kupepeta KCB 32-20 ugani RFUEA jijini Nairobi, Jumamosi.
Chini ya kocha Carlos Katywa kutoka Afrika Kusini, wanasukari wa Kabras walipata pointi zao kupitia wachezaji Ntabeni Dukisa (mikwaju mitatu, penalti moja na mguso) na Humphrey Asiligwa, James Olela na Eugene Sifuna (mguso mmoja kila mmoja).
Wanabenki wa KCB walifunga alama zao kupitia kwa chipukizi Michael Wamalwa (mguso), Shaaban Ahmed (mguso), Levy Amunga (mkwaju), Festus Shiasi (mkwaju) na Elvis Namusasi (penalti mbili).
Vijana wa kocha Curtis Olago, KCB, walikamilisha mechi wachezaji 14 baada ya Namusasi kuonyeshwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya kabla tu ya kipindi cha kwanza kutamatika.
Kabras walishinda Enterprise Cup kwa mara ya kwanza mwaka 2019 kabla ya kuongeza mataji ya mwaka 2022, 2023 na 2024. Makala ya 2020 na 2021 yalivurugwa na janga la virusi vya corona.
Washindi wa mashindano ya Enterprise Cup:
1930 Nairobi District
1931 Nairobi North
1932 West Kenya
1933 Eldoret
1934 Eldoret
1935 Eldoret
1936 Eldoret
1937 Nondescripts RFC
1938 Nondescripts RFC
1939 Eldoret
1940 Hayakuchezwa kutokana na Vita Vikuu vya Dunia
1941 Hayakuchezwa kutokana na Vita Vikuu vya Dunia
1942 Hayakuchezwa kutokana na Vita Vikuu vya Dunia
1943 Hayakuchezwa kutokana na Vita Vikuu vya Dunia
1944 Hayakuchezwa kutokana na Vita Vikuu vya Dunia
1945 Hayakuchezwa kutokana na Vita Vikuu vya Dunia
1946 Hayakuchezwa kutokana na Vita Vikuu vya Dunia
1947 Eldoret
1948 Nakuru
1949 Nondescript RFC
1950 Nondescript RFC
1951 Nondescript RFC
1952 Coast Province
1953 West Kenya
1954 Nondescript RFC
1955 Kenya Harlequin FC
1956 Kampala RFC
1957 Kenya Harlequin FC
1958 Nakuru RFC
1959 Kenya Police RFC
1960 Nakuru RFC
1961 Impala RFC
1962 Nakuru RFC
1963 Nakuru RFC
1964 Kenya Harlequin FC
1965 Impala RFC
1966 Nondescripts RFC
1967 Kitale RFC
1968 Kampala RFC
1969 Kampala RFC
1970 Kampala RFC
1971 Impala RFC
1972 Impala RFC
1973 Impala RFC
1974 Impala RFC
1975 Nondescripts RFC
1976 Nondescripts RFC
1977 Nondescripts RFC
1978 Nondescripts RFC
1979 Nondescripts RFC
1980 Nondescripts RFC
1981 Nondescripts RFC
1982 Nondescripts RFC
1983 Nondescripts RFC
1984 Nondescripts RFC
1985 Mwamba RFC
1986 Mwamba RFC
1987 Hayakuchezwa kutokana na Michezo ya Afrika
1988 Kenya Harlequin FC
1989 Nondescripts RFC
1990 Nondescripts RFC
1991 Nondescripts RFC
1992 Nondescripts RFC
1993 Nondescripts RFC
1994 Nondescripts RFC
1995 Kenya Harlequin FC
1996 Kenya Harlequin FC/Nondescripts RFC
1997 Mombasa Sports Club
1998 Nondescripts RFC
1999 Kenya Harlequin FC
2000 Impala RFC
2001 Impala RFC
2002 Impala RFC
2003 Impala RFC/Kenya Harlequin FC
2004 KCB RFC
2005 Impala RFC
2006 Mwamba RFC
2007 KCB RFC
2008 Nakuru RFC
2009 Kenya Harlequin FC
2010/11 Kenya Harlequin
2011/12 Hayakuchezwa
2012/13 Mwamba RFC
2013/14 Nakuru RFC
2014/15 KCB RFC
2015/16 KCB RFC
2016/17 KCB RFC
2017/18 Homeboyz RFC
2018/19 Kabras Sugar
2019/20 Hayakuchezwa kutokana na Covid-19
2021 Hayakuchezwa kutokana na Covid-19
2022 Kabras Sugar
2023 Kabras Sugar
2024 Kabras Sugar