• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:55 AM
Jopo la kufufua sekta ya sukari kuanza vikao

Jopo la kufufua sekta ya sukari kuanza vikao

Na VITALIS KIMUTAI

MAGAVANA wa Kaunti zinazokuza miwa katika Magharibi mwa nchi, wiki hii wataandaa mikutano na viongozi waliochaguliwa, wakulima na wadau wengine kutoka maeneo katika juhudi za kufufua viwanda vya sukari vilivyoporomoka.

Wanachama wa majopo ya pamoja kutoka serikali ya kitaifa na Muungano wa Kiuchumi wa Kaunti za Ziwa Viktoria watakutana na maseneta, wabunge wakilishi wa wanawake, na wabunge ili kutatua masuala yanayoendelea kuwaathiri wakulima wa miwa, viwanda vya sukari na wafanyabiashara katika sekta ya kilimo cha miwa.

Hata hivyo, baadhi ya wakulima wamedai kwamba mikutano hiyo haitakuwa na maana kwa kuwa baadhi ya maamuzi kuhusu masuala yanayoaathiri sekta ya sukari yanaonekana yalishafanywa kitambo na vikao hivyo ni vya kupoteza muda na rasilimali.

Kulingana na mwekahazina wa kitaifa wa chama cha kitaifa cha wakulima wa miwa, Stephen Marupa, vikao hivyo huenda vikakosa kuwanufaisha wakulima kwa sababu hawajahusishwa vilivyo.

“Mawasilisho yetu kwa majopo hayo yanazua maswali kwa sababu tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wa majopo hayo wamehusika katika utoaji wa leseni za kuagiza sukari kutoka nje, na hivyo kuchangia kuporomoka kwa viwanda vyetu,” akaelezA Bw Narupa.

“Tunaunga mkono Rais Uhuru Kenyatta katika juhudi zake za kufufua sekta ya sukari, lakini tuna hofu kwa sababu baadhi ya wanachama wa jopo alilobuni ndio chanzo cha masaibu ya wakulima wa miwa,” akaongeza Bw Narupa.

Mwezi Novemba mwaka jana, serikali ilitangaza jopo la wanachama 14 kuandaa ripoti kuhusu changamoto zinazokabili sekta ya sukari kama njia ya kuinusuru sekta hiyo.

Waziri wa Kilimo, Mwangi Kiunjuri na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya wanaongoza jopo hilo ambalo wanachama wake wengine ni magavana Okoth Obado wa Migori na Prof Anyang Nyong’o wa Kisumu wanaowakilisha baraza la magavana.

Wakiwa mjini Kisii, Bw Oparanya alitangaza kwamba wataanza misiruru ya ziara na mikutano katika viwanda vyote vya sukari hapo Jumatano ili kuzungumza na wakulima wakilenga kupata mapendekezo muhimu yatakayosaidia kuikwamua sekta hiyo iliyokuwa ikinawiri, na kuwa kitega uchumi kwa wakazi wa maeneo hayo.

Bw Oparanya vile vile alimwomba Bw Kiunjuri kuwalipa wakulima wa miwa deni la Sh2.6 bilioni jinsi alivyoamrisha Rais Kenyatta mwaka jana.

You can share this post!

Ushauri wa Gathoni wa Muchomba kuhusu 2022

Serikali kutathmini deni la Sh2b kufichua wanakandarasi hewa

adminleo