Uchina yafanikiwa kukuza mimea kwa mwezi
MASHIRIKA Na PETER MBURU
UCHINA imefanikiwa kupanda mimea kwenye mwezi kwa mara ya kwanza katika historia, baada ya mimea ya pamba ambayo ilipanda kumea.
Katika picha ambazo shirika la China National Space Administration (CNSA) lilituma Jumanne, mbegu za pamba ambazo zilipandwa kwenye mwezi zilionekana kuanza kumea, ishara nzuri kuwa sayari hiyo inaweza kuwezesha maisha.
Shirika hilo lilisafirisha mbegu za mimea tofauti kufanya jaribio hilo, zingine zikiwa za viazi na mimea iitwayo oilseed rape, Arabidopsis, yeast na fruit flies.
Mimea Zaidi inatarajiwa kukua humo kwa kipindi cha siku 100 zijazo, shirika hilo likasema.
Picha hiyo ilichapishwa katika tovuti ya Chuo Kikuu cha Chongqingm ikisema “Baada ya kufanya majaribio ya hewa ya mwezi tofauti kubwa za joto, miale mikali na mazingira magumu, binadamu amekuza mmea wa kwanza, kutambua kitu cha binadamu cha kwanza kukua katika mwezi.”
Hata hivyo, hakuna mmea mwingine kati ya mingine iliyosafirishwa ambao umekua, chuo hicho kikasema.
Mimea iliyoteuliwa inatarajiwa kuonyesha wanasayansi uwezo wa anga ya mwezi kuwezesha kilimo kufanyika, katika vizazi na vizazi vya mimea.
Anga ya mwezi hupata joto la hadi digrii 127 na baridi kwenda hadi digrii -173.
Wanasayansi hao wanatarajia kuwa mbegu za viazi na Arabidopsis zitamea na kunawiri mwezini kwa siku 100, huku kila kitu kikirekodiwa kwa kamera na kupeperushwa hadi kwa Dunia.