Pacha waungama kushiriki ngono na mpenzi mmoja

MASHIRIKA Na PETER MBURU

PACHA wawili kutoka Australia wametoboa kuwa wamekuwa wakishiriki ngono na mpenzi wao mmoja kwa zamu, kwa miaka minane sasa.

Wawili hao ambao wana miaka 33 kutoka Jiji la Perth walisema kuwa kwa muda huo, kila wakati mmoja wao anapokuwa akishiriki mahaba na mpenzi wao Ben Byrne, mwenzake huwa hapo.

Wawili hao walitoboa hayo katika kipindi cha runinga, ambapo walisema kuwa walianza uhusiano na Ben tangu 2012.

Walisema “huwa tunalala katika kitanda cha kifalme, kikubwa kuliko cha kifalme hata kwa inchi sita.”

Walisema kuwa huwa kila mmoja wao analala upande mmoja wa Ben. “Hakuna wivu katika uhusiano wetu, Ben akimbusu Anna, pia atanibusu mimi,” Anna, mmoja wao akasema.

Dada hao walieleza kuwa wangependa kufunga ndoa na mpenzi wao wa muda mrefu, japo kisheria, ndoa ya zaidi ya mke mmoja imepigwa marufuku huko Australia.

Wawili hao walisema kuwa kwa kuwa huwa wanafanya kila kitu kwa pamoja kama kula na kunywa, hata choo huwa wanaenda kwa wakati mmoja.

Walisema kuwa hata wanapanga kuwa waja wazito kwa wakati mmoja, wakisema ni kazi ya Ben mpenzi wao kuhakikisha kuwa hilo linatimia.

Dada hao walifahamika kwa mara ya kwanza walipotumia mamilioni ya pesa kufanyiwa matibabu ya kuwafananisha kabisa.

“Ikiwa tunaweza kubadili sheria na serikali, tungependa kumuoa Ben. Mapenzi ni mapenzi, sote ni watu wazima na tunafaa kuoa mwanamume sawa,” akasema Anna.

Habari zinazohusiana na hii