Wanaharakati wa mazingira 142 waliuawa 2024-Ripoti
WANAHARAKATI wa mazingira wasiopungua 142 waliuawa kote duniani mwaka uliopita na wengine wanne hawajulikani waliko.
Hii ni kulingana na ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali la Global Witness.
Ripoti hiyo inasema wengi ya waliolengwa walikuwa wakipigania haki za wakulima wadogo.
Wengine ni pamoja na wale waliokuwa wanapambana dhidi ya uchimbaji haramu wa madini, biashara ya magogo, ujangili na miradi ya nishati.
Kulingana na ripoti, kwa mara nyingine Colombia imeongoza kwa idadi kubwa ya vifo 48 vya wanaharakati wa mazingira ikifuatiwa na Guatemala, Mexico na Brazil.
Watafiti wamesema mauaji mengi yalifanywa na makundi ya wahalifu na katika baadhi ya matukio vyombo vya usalama wa taifa vilihusika.