Habari MsetoSiasa

Lonyangapuo awataka walionyakua ardhi ya umma wairejeshe upesi

February 20th, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na OSCAR KAKAI

GAVANA wa Pokot Magharibi, Prof John Lonyangapuo ameaonya vikali wanyakuzi wa ardhi na wanaohusika na ufisadi katika kaunti hiyo.

Gavana huyo amewataka wale ambao wamenyakua ardhi ya umma kuirejesha kwa serikali ama waondolewe kwa kutumia nguvu.

“Tumewapa wiki moja warejeshe ardhi ama tuwaaname kwa kuwa hakuna aliyezidi sheria,” alisema.

“Hatutaendelea kucheka na wezi ambao wamekuwa wakiwanyanyasa wakazi ,” alisema Prof Lonyangapuo akiwa mjini Kapenguria akikagua miradi ya maendeleo.

,Prof Lonyangapuo alisema kuwa ardhi kubwa katika kaunti hiyo imenyakuliwa na mabwenyenye .“Hatutajali wewe ni nani bora uwe umechukua ardhi ya umma tutakabiliana na wewe vilivyo,” alisema.

Aliwataka wale ambao wana mashamba ya umma kuyarejesha maramoja kabla ya hatua kali kuchukuliwa.

“Tutachukua mashamba yote ambayo yako mikononi mwa watu binafsi,” alisema.

Kiongozi huyo alisema kwua hatakubali maovu kutendeka wakati wa uongozi wake.

“Mashamba ya umma yanafaa kunufaisha wakazi na wala sio watu binafsi ,” alisema.

Prof Lonyangapuo alisema kuwa watu hao wanafaa kuwa siku zao zimekwisha huku akisema kuwa wengi wamenyakua mashamba karibu na ofisi za serikali .

Alisema kuwa serikali ya kaunti hiyo itawapokonya hati miliki za mshamba wale ambao walinyakua huku akisema kuwa wana biashara wengi wamechukua mali nyingi ya umma.

“Kuna mijengo ambayo imejengwa kwa ardhi ya umma .Tunataka kujua mahali alipata ardhi hiyo ya umma,” alisema Prof Lonyangapuo.

Prof Lonyangapuo alisema makataa yametolewa kwa wati ambao wanaishi kwenye mashamba ya umma katika miji tofauti katika kaunti hiyo na serikali ya kaunti itawaondoa.? “Serikali yangu itafanya kila jambo kulinda haki za wakazi na kuchunga mali yao,” alisema.

Aliwataka wanyakuzi kuondoka huku akisema kuwa serikali yake ina mipango ya kupanga umpya mji wa Kapenguria ili wakazi wapate huduma bora.? “Hatuwezi kujenga mabanda ndani ya mji ambapo watu watapata wakati mgumu wakati mkasa umetokea,” alisema.

Vile vile ,kiongozi huyo aliwaonya wale ambao wanahusika na ufisadi akisema kuwa siku zao zimekwisha.

Prof Lonyangapuo alisema kuwa tayari amewasimamisha kazi maafisa wawili kazi akiwemo afisa wa uajiri katika kaunti hiyo huku uchunguzi ukiendelea kufanywa.

“Hatuchezi na wafisadi na tutafuata mkondo wa Rais,” alisema