Kimataifa

Watu 31 wauawa kufuatia makabiliano kati ya jeshi na wanamgambo

Na REUTERS November 20th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

JESHI la Mali limewaua wanakijiji 31 katika mashambulio dhidi ya vijiji viwili vya Mkoa wa Segou ambapo kundi kuu la waasi lenye uhusiano na al Qaeda linaendesha shughuli zake.

Hii ni kulingana na ripoti iliyotolewa Novemba 19, 2025 na shirika la Human Rights Watch.

Kulingana na ripoti hiyo, watu 10 wakiwemo mwanamke mmoja waliuawa katika kijiji cha Balle.

Mashahidi walielezea kuwa vikosi vya jeshi na wanamgambo vilikabiliana baada ya taarifa kutolewa kuwa wanakijiji walikuwa wakishirikiana na Jama’at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM).

Kundi linaloshirikiana na al Qaeda limepanua operesheni zake kusini mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Mashahidi hao ni pamoja na mchungaji wa eneo hilo ambaye alinusurika baada ya kujificha katika nyumba iliyotelekezwa na bintiye mwenye umri wa miaka tisa, na baadaye kupata miili 17 ikiwa na risasi, shirika la HRW lilisema.

Umoja wa Afrika na msemaji wa jeshi la Mali hawakujibu mara moja ombi la shirika la habari la Reuters kuhusu ripoti hiyo.

Umoja wa Afrika umesema utachukua hatua za kusaidia kumaliza mzozo huo na kuwawajibisha wahusika kwa uhalifu huo.

Mali iko chini ya shinikizo kutoka kwa makundi ya wanajihadi ambayo yamekuwa yakishambulia vikosi vya serikali na katika miezi ya hivi karibuni iliweka kizuizi cha mafuta ambacho kimesababisha foleni ndefu kwenye vituo vya mafuta na kufanya upatikanaji wa jenereta za dizeli kuwa ghali zaidi.Waziri wa mambo ya nje wa Mali wiki hii alipuuzilia mbali madai kwamba hakuna uwezekano wa kuchukua udhibiti wa mji mkuu wa Bahari.