Ebola: Amerika yaongeza tahadhari kwa wanaosafiri Kenya
AMERIKA Jumatatu jioni ilipandisha kiwango cha tahadhari ya usafiri kwa Kenya kutoka hadhi ya pili hadi ya tatu (Level Two hadi Level Three) ikiwasihi raia wake kufikiria upya mipango ya kutembelea nchi hii.
Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na hatari za kiafya na kiusalama dhidi ya maambukizi ya Ebola.
Kupitia taarifa, Wizara ya Masuala ya Nje Amerika ilitaja hatari ya Ebola, uhalifu, utekaji nyara, ugaidi, machafuko ya raia na usalama barabarani kama baadhi ya sababu za tahadhari hiyo.
Kenya imethibitisha kisa kingine cha Ebola, na kufanya jumla ya visa kufikia vinane.
Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Dkt Patrick Amoth, alisema watu 38 walipimwa Jumapili, ambapo mmoja alipatikana na virusi vya aina ya Bundibugyo. Kisa hicho kilikuwa cha mhudumu wa afya aliyekuwa akiwaangalia wagonjwa.