• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Messi awaokoa Barca dhidi ya Nari Villareal

Messi awaokoa Barca dhidi ya Nari Villareal

Na MASHIRIKA

BARCELONA, Uihspania

ILIBIDI kocha Ernesto Valverde wa Barcelona amuingize staa Lionel Messi kusaidia kikosi chake kilichokuwa kikipondwa na Villarreal kabla ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya 4-4.

Villarreal walikuwa juu kwa 4-2 kabla ya Luis Suarez na Messi kupachika wavuni mabao mawili mechi hiyo ikielekea kumalizika ugani Nou Camp.

Licha ya sare hiyo, Barcelona wanabakia uongozini kwa pengo la pointi nane mbele ya Atletico Madrid ambao waliandikisha ushindi wa 2-0 dhidi ya Girona.

Wakianza bila Messi, Gerard Pique na Ivan Rakitic, Barcelona walitangulia kupata bao kupitia kwa Philippe Coutinho dakika ya 12, kabla ya Malcon kuongeza la pili.

Villarreal ambao walianza mechi hiyo wakiwa katika mduara wa kushushwa daraja, walipata bao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Samuel Chukwuze.

Fowadi Lionel Messi wa FC Barcelona afunga bao Barca ilipokabiliana na Villarreal CF AprilI 2, 2019, uwanjani Ceramica. Picha/ AFP

Mshambuliaji Karl Toko Ekambi wa Cameroon alipenya ngome ya Barca na kupachika wavuni bao la kusawazisha baada ya kumzidi maarifa kipa Marc-Andr’e ter Stegan kabla ya Vicente Iboora kuongeza la tatu.

Carlos Bacca aliifungia Villarreal bao la nne na kufanya mambo kuwa 4-2.

Ni mechi ambayo mashabiki walishuhudia kadi nyekundu ikitolewa kwa Alvaro Gonzalez zikibakia dakika nne mechi kumalizika, hali iliyochangia kikosi kulegea na baadaye kuchangia kupatikana kwa mabao mawili ya haraka.

Nchini Italia, licha ya kurushiwa matusi ya kiubaguzi kutoka kwa mashabiki wa Cagliari, mshambuliaji Moise Kean hatimaye aliifungia Juventus bao katika ushindi wao wa 2-0.

Baada ya kufunga bao, Kean -ambaye ni raia wa Italia aliyezaliwa na raia wa Ivory Coast alikimbilia mashabiki wa nyumbani na kukunja mikoni yake huku akiwapungia, kitendo ambacho kiliwaudhi mashabiki wa Cagliari walioanza kumpigia kelele huku wakimvurumishia matusi ya kila aina.

Matuidi alalamika

Wakati mmoja, kiungo Blaise Matuidi wa Juventus alilalamikia vikali kitendo hicho huku akitishia kuondoka uwanjani.
Mfaransa huyo aliwahi kufanyiwa hivyo katika mechi ya awali, lakini klabu ya Cagliari iliomba msamaha.

Mechi ilisimaishwa kwa dakika tatu na ikabidi watangazaji wa uwanjani watoe onyo kali.

Hata hivyo, Leonardo Bonuucci alimlaumu Kean kwa kusherehekea akiwaangalia mashabiki badala ya kufurahia bao hilo akiwa na wenzake.

Mlinzi Bonucci alitangulia kufungia Juventus bao la kwanza kwa kichwa kufuatia kona dakika ya 22.

Juhudi za vinara hao kuongeza mabao zaidi zilizimwa na kipa matata Alessio Cragno.

Ushindi huo umeipatia Juventus jumla ya ponti 81 kutokana na mechi 30, pointi 18 mbele ya Napoli waliotarajiwa kucheza na Empoli jana usiku.

Kwa mara nyingine, Juventus walicheza bila Cristiano Ronaldo aliyeumia paja akichezea timu ya taifa ya Ureno, wiki iliyopita.

Tukirejelea ligi kuu ya La Liga, Atletico Madrid walicharaza Girona 2-0 kutokana na mabao ya Diaego Godin na Antoine Grienzmann.

You can share this post!

Kariobangi Sharks kuonana na Zoo huku Ingwe ikiikabili...

Manchester United ingali na matumaini

adminleo