• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 6:55 PM
Wizara ya Afya yasema haijui ziliko Sh11 bilioni

Wizara ya Afya yasema haijui ziliko Sh11 bilioni

Na BERNARDINE MUTANU

Wizara ya Afya imeshindwa kuelezea zilikoenda au zilivyotumiwa Sh11 bilioni ilizopewa.

Ripoti hii ni kwa mujibu wa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Bw Edward Ouko.

Pesa hizo ni pamoja na Sh10 bilioni ilizopewa Wizara ya Huduma za Matibabu na Wizara ya Afya kabla ya kuunganishwa 2013.

Pesa hizo hazikuwasilishwa na kuwekwa katika akaunti moja na mpya baada ya wizara hizo kuunganishwa.

Ripoti hiyo inaelezea pia kuwa Sh1.3 bilioni hazikutumiwa ilivyofaa. Pesa hizo zililipwa vifaa na huduma ambazo hazikutolewa kama vile kliniki za kontena, dawa, vifaa vya matibabu na upanuzi wa hospitali.

Kulingana na ripoti hiyo ya 2015/16, wizara hiyo ilikuwa na madeni ya Sh2.4 bilioni kufikia Juni 30, 2016.

Madeni hayo yalisongeshwa hadi 2017, kulinga na Bw Ouko.

You can share this post!

Pesa zenu zi salama, KCB yawahakikishia wateja...

Kenya ina mabilionea 180 na mamilionea 1290 – Knight...

adminleo