• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Wapenzi wajiua waache kuchafua dunia kwa kupumua CO2

Wapenzi wajiua waache kuchafua dunia kwa kupumua CO2

MASHIRIKA Na PETER MBURU

WANANDOA kutoka California walijitoa uhai wiki hii kama mbinu ya kuokoa dunia kutokana na ongezeko la joto na kubadilika kwa mazingira.

Dove Sweetwater wa miaka 13 na Dusk Lennon wa miaka 32 walielewana kujiua pamoja na marafiki zao kadhaa, kabla yao kufanya hivyo.

Wapenzi hao walipatana na kupendana mnamo 2018 katika hafla moja eneo la Arcata, mwaka tu kabla ya kuchukua hatua hiyo.

Japo walikuwa wameelewana pamoja na marafiki wengine 23 kujiua kwa sababu hiyo, ni wapenzi hao wawili tu ambao walitekeleza ahadi, na wakajiua.

“Nawezaje kuwa mzigo katika dunia hii wakati tunatoa hewa chafu (CO2) katika maisha yetu kwa kupumua, kunyamba na kutoa hewa kwa njia nyingine?” Dove Sweetwater akasema katika barua aliyoandikia wazazi wake.

Watu wa familia ya Sweetwater aidha wanaamini kuwa hali kuwa aligundua alikuwa na uja uzito wa mpenzi wake Dusk Lennon siku chache zilizopita huenda ndiyo ilimsukuma kuchukua hatua hiyo.

Walisema hawawezi kuchangia katika uchafuzi wa mazingira kwa kupumua, na wakaona kuwa suluhisho ya pekee ilikuwa kujiondoa uhai, ili wasipumue tena.

Ripoti ya shirika la Rockfeller Foundation mnamo 2017 ilibaini kuwa hewa ya CO2 ambayo inatolewa na binadamu kwa kupumua na kunyamba ndiyo inachangia vikubwa zaidi kuongezeka kwa joto duniani.

Ripoti hiyo aidha ilisema kuwa ili kupunguza kiwango cha kuongezeka kwa joto katika dunia, itabidi idadi ya binadamu kupungua kutoka bilioni saba ya sasa, hadi milioni 500, kufikia 2050.

You can share this post!

Maafisa wa mbuga wadai Sh1.9 milioni zilizopotea zilimezwa...

Watu 100 watuma maombi ya kazi ya kuua wahalifu

adminleo