• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 4:48 PM
Oburu Odinga aikejeli EACC kwa kumpokonya ardhi

Oburu Odinga aikejeli EACC kwa kumpokonya ardhi

Na RUSHDIE OUDIA

MBUNGE wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Oburu Oginga ameishutumu Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kwa kumpokonya ardhi yake iliyorejeshwa kwa Shirika la Reli nchini (KRC).

Bw Oburu alidai kuwa alilengwa kimakosa kwa sababu yeye ni ndugu ya kiongozi wa Upinzani Raila Odinga.

Mbunge huyo aliitaka tume ya EACC kushughulikia sakata kubwa zinazohusiana na wizi wa mabilioni ya fedha za walipa ushuru na kukoma kuandama watu wadogo kama yeye.

Alisema kuwa mahakama ilikuwa imemwondolea lawama kutokana na madai kwamba alinyakua ardhi ya serikali.

Tume ya EACC ilimpokonya Bw Oburu kipande hicho cha ardhi huku ikisema kuwa alipewa kinyume cha sheria ardhi iliyomilikiwa na Shirika la Reli.

Tume ya EACC pia ilitwaa kipande cha pili kilichokuwa kimenyakuliwa na kampuni ya Kendeep Construction.

Mkurugenzi Mkuu wa EACC Twalib Mbarak Ijumaa iliyopita aliapa kuwa atahakikisha kuwa ardhi iliyonyakuliwa katika Kaunti ya Kisumu inarejeshwa.

Vipande vyote viwili vya ardhi vilivyorejeshwa vina thamani ya Sh60 milioni, kulingana na EACC.

You can share this post!

Waiga sauti za fisi ili kuiba mifugo usiku bila bughudha

Kalonzo, Mudavadi wamtetea Uhuru

adminleo