• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Wazee wataka mkewe Ken Okoth ‘arithiwe’ kulingana na mila

Wazee wataka mkewe Ken Okoth ‘arithiwe’ kulingana na mila

Na PETER MBURU

BARAZA la wazee katika jamii ya Luo sasa linawataka mama na mjane wa mbunge wa Kibra aliyeaga dunia majuzi Ken Okoth kusafiri hadi nyumbani kwao katika mtaa wa Kabondo, Kaunti ya Homa Bay, ili kufanyiwa utamaduni kufuatia kifo cha mbunge huyo.

Mwenyekiti wa baraza hilo Nyandiko Ongadi Jumapili alisema kuwa wawili hao, Monica Okoth (mjane wa Ken Okoth) anafaa kuandamana na mavyaa wake hadi nyumbani kwao kwa utamaduni huo, pamoja na ‘kurithiwa’ kulingana na matakwa ya jamii ya Luo.

Bw Ongadi, hata hivyo, alilaumu hatua ya maiti ya mbunge huyo kuteketezwa, akisema ndiyo ya kwanza na mbaya zaidi kuwahi kutendeka katika jamii ya Luo.

Alisema hivyo baada ya maiti ya Bw Okoth kuchomwa Jumamosi alfajiri, katika kaburi la kuteketezea maiti mtaani Kariokor, jijini Nairobi.

Wakazi nyumbani kwa kina mbunge huyo eneo la Kabondo walikuwa wakisubiri maiti yake kwa ajili ya mazishi Jumamosi, lakini wakapata habari kuwa aliamkia kuchomwa, kulingana na wosia wake.

You can share this post!

Ufugaji ajira ya maana baada ya kustaafu, Sh165,000 kila...

Kuteua ‘mipango ya kando’ kwa afisi za serikali...

adminleo