• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Twitter yajiunga na Google na Facebook kuharamisha matangazo ya Bitcoin

Twitter yajiunga na Google na Facebook kuharamisha matangazo ya Bitcoin

Na BERNARDINE M UTANU

KAMPUNI ya mtandao wa kijamii ya Twitter imepiga marufuku matangazo ya sarafu za siri (cryptocurrency).

Kampuni hiyo ilitangaza kuwa kuanzia Jumanne, hakutakuwa na matangazo ya sarafu hiyo katika mtandao wake.

Imejiunga na kampuni zingine zinazoendesha biashara zake kupitia kwa intaneti kama vile Facebook na Google katika hatua ya kukabiliana na udanganyifu au hasara miongoni mwa wawekezaji.

Katika soko la mtandaoni, kuna sarafu 1587 za siri ambazo ‘huchimbwa’ na kugeuzwa pesa halisi. Mifano ni Bitcoin, Ethereum, Ripple, Bitcoin Cash, Litecoin na Cardano.

Marufuku hiyo inanahusu ofa ya kwanza ya sarafu (ICOs) na mauzo, ilisema kampuni hiyo wakati wa mahojiano na Reuters Jumatatu.

Kampuni hiyo imepiga marufuku pia biashara za kampuni za sarafu hizo kutangaza biashara zao ikiwa hazijaorodheshwa katika soko la hisa linalofahamika.

Mpango huo utatekelezwa katika muda wa siku 30 zijazo. Kuanzia Juni, hakutakuwa na matangazo hayo kwa Google baada ya kampuni hiyo kupiga marufuku.

Facebook kwa upande wake imedhibiti matangazo hayo katika mtandao wake.

You can share this post!

Murang’a ndiyo kaunti fisadi zaidi Kenya –...

Mabwanyenye wachache wanamiliki 80% ya utajiri Nairobi na...

adminleo