• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Ujenzi wa soko la Githurai waanza

Ujenzi wa soko la Githurai waanza

Na SAMMY WAWERU

UJENZI wa soko la Githurai maarufu kama Jubilee Market na lililoko eneobunge la Ruiru, Kaunti ya Kiambu, umeanza.

Aidha, hughuli hizo zinafadhiliwa na serikali ya kitaifa. Rais Uhuru Kenyatta akifanya kampeni 2017 kutetea kuhifadhi kiti chake kwa awamu ya pili na ya mwisho aliahidi wakazi wa mtaa huo kuwajengea soko la ghorofa na lenye egesho la magari.

Septemba 28, 2019, naibu gavana wa Kiambu James Nyoro na mbunge wa Ruiru Simon King’ara waliongoza hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa awamu ya kwanza.

“Hii ni mojawapo ya ahadi ya serikali kufanyia wakazi wa eneo hili maendeleo,” akasema Bw Nyoro ambaye kwa sasa ni kaimu gavana.

Mbunge wa Ruiru Simon King’ara akionesha cheti cha uzinduzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko la Githurai. Picha/ Sammy Waweru

Kufuatia madai ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha yanayomsibu gavana Ferdinand Waititu, mahakama iliamuru asiingie ofisini.

Wakati wa uzinduzi wa soko hilo, King’ara alisema awamu ya kwanza itagharimu kima cha Sh800 milioni. “Awamu ya kwanza ikikamilika, itasitiri zaidi ya wafanyabiashara 2,000” akasema mbunge huyo. Alisema mwanakandarasi aliyepewa ujenzi huo anatakiwa kuajiri vijana wa eneo la Githurai.

Mwaka 2018  ubomoaji wa vibanda ulifanyika wafanyabiashara wakitakIwa kutengeneza vile tamba.

Waititu alisema ujenzi wa mradi huo utagharimu Sh4 bilioni.

Wasiwasi wa wafanyabiashara

Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara wana walakini na jakamoyo kuhusu ugavi wa majumba soko litakapokamilika.

“Suala la ubaguzi na wenyeji kuondolewa kwenye masoko yanapoimarishwa si geni nchini. Tunaomba mikakati kabambe iwekwe ili kuwapa nafasi ya kwanza tuliokuwepo,” mfanyabiara Samson Gitau akaambia Taifa Leo.

Eneo linalopaniwa kujengwa soko la Githurai lina ukubwa wa karibu ekari nne.

You can share this post!

AKILIMALI: Ufugaji ng’ombe haukumpa faida...

RIZIKI NA MAARIFA: Amekuwa na wengi mifugo, lakini aungama...

adminleo