Michezo

Coca-Cola yatoa Sh42 milioni kushindaniwa na Wakenya wakisubiri Kombe la Dunia

April 5th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na CHRIS ADUNGO

KAMPUNI ya vinywaji ya Coca-Cola  itawatuza watumiaji  wa bidhaa zake milioni mbili, mwaka huu katika kipute cha Kombe la Dunia unaopangiwa kuanza mwezi Juni  nchini Urusi.

Katika kampeni yake ya Funga Mamili na Coca-Cola, watakaotumia bidhaa zao kwa wiki kumi na sita zijazo watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali za thamani ya Sh42.5 milioni.

“Coca-cola imekuwa mdhamini wa Kombe la Dunia kwa zaidi ya miongo minne sasa. Katika matayarisho ya kombel hili la FIFA, tunalenga kutumia msisimko wa Wakenya wanaopenda soka na kuwazawadi  kupitia kampeni hii.

Zawadi hizo zinawapa nafasi mbalimbali za kujitayarishia mchezo huo kwa kuwafanya watu  millionia kumi na sita mamilionea mwishoni mwa kampeni hio,”  akasema Rodney Nzioka mwadamizi, meneja wa brandi ya kampuni hiyo.

Bidhaa zitakazotumiwa katika ukuzaji  huu ni pamoja na soda za Coca-cola, Sprite, Krest na Stoney zitakazokuwa kwa chupa za plasitiki ama kioo ambazo  zitakuwa  na kifuniko cheupe zitakazopatikana madukani  kote nchini.

Pesa taslimu za kushindaniwa ni kati ya shilingi mia tano na milioni moja,  zawadi zinginezo zikiwa runinga za dijitali, vifushi vya data, na malipo ya runinga.

Watakaoshiriki lazima wawe wamajisajili kama watumiaji wa huduma za simu za mkononi  za mitandao ya Safaricom, Airtel, Telkom na Yu.

Kushiriki unahitajika kutuma nambari  nane kwenye kifuniko kwa nambari 40111 ili kupata nafasi ya kujishindia  zawadi kila siku na kila wiki.