• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Dow yashirikiana na ChildFund kuwapa watoto motisha kuhifadhi mazingira

Dow yashirikiana na ChildFund kuwapa watoto motisha kuhifadhi mazingira

Na MAGDALENE WANJA

KATIKA juhudi za kuwaweka watoto katika hali ya wao kujenga mazoea ya kutunza mazingira, kampuni ya Dow Chemical imeshirikiana na ChildFund ambao ni wakfu unaohusika na maswala ya watoto.

Ushirikiano huo utawawezesha watoto hao kuwa mabalozi wa maswala ya mazingira kupitia mradi wa kampuni ya Dow unaojulikana kama Project Butterfly.

Project Butterfly ni mradi ulioanzishwa Oktoba 2017 Tembisa nchini Afrika Kusini na ulitokana na msukumo wa kubadilisha taka za plastiki kuwa vitu vinavyovutia.

Mradi huo nchini ulianzishwa katika makazi duni ya Mukuru mnamo mwaka 2018.

Washirika wa mradi huo wamekuwa wakijihusisha na baadhi ya miradi kama vila kusafisha mazingira katika mitaa mbalimbali jijini Nairobi.

Kulingana na naibu mkuu katika kitengo cha Upakiaji na Plastiki Maalum – Packaging and Specialty Plastics – katika kampuni ya Dow, Marco Ten Bruggencate, usafishaji mazingira ni mojawapo ya miradi ambayo kampuni hiyo imekuwa ikifanya.

“Bara la Afrika linakua kwa kasi na inakadiriwa kuwa miaka 30 ijayo kutakuwa na ongezeko la watu bilioni tatu na hivyo changamoto ya taka inafaa kuwa na suluhisho kufikia sasa,” akasema Bruggencate.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la ChildFund nchini Kenya Bi Chege Ngugi alisema kuwa mpango huo utafanya vyema zaidi kwa kushirikiana na miradi mingine ya hapo awali kama vile Mazingira Bora Project katika eneo la Mukuru.

“Kupitia ushirikiano kama huu baina ya mashirika binafsi na ya serikali, Kenya itaweza kupata suluhu katika maswala ya utupaji taka,” akasema Bi Ngugi.

You can share this post!

Tume kuhusu haki yaitaka serikali kutumia mbinu za kiutu Mau

Ripoti ya BBI tayari kupakuliwa

adminleo