• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 3:25 PM
Msomi Mkenya apewa miezi 3 kuondoka Amerika

Msomi Mkenya apewa miezi 3 kuondoka Amerika

Na CHRIS WAMALWA

MKENYA mmoja msomi ambaye amekuwa akizozana na idara ya uhamiaji Amerika kwa muda mrefu amepewa makataa ya miezi mitatu kuondoka nchini humo baada ya kupoteza kesi ya kupinga kufurushwa kwake.

Profesa Aggrey Mbenga Wanyama, binamu ya Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa alipewa makataa hayo Alhamisi wiki iliyopita.

Prof Wanyama sasa atarejeshwa Kenya kwa nguvu ikiwa atakataa kuondoka Amerika kabla ya Julai 14 baada ya kuishi na kufanyakazi nchini humo kwa zaidi ya miaka 25.

Msomi huyo, ambaye ni Profesa wa somo la Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Augsburge jimboni Minnesota, Alhamisi alifeli kupata kibali cha kuendelea kuishi Amerika.

Runinga ya CBS iliripoti kwamba, maafisa wa Idara ya Uhamiaji na Forodha walimwambia msomi huyo mzaliwa Kenya kwamba, ombi lake la kutaka kuruhusiwa kuendelea kuishi na kufanyakazi Amerika lilikataliwa.

“Kwa hivyo, Prof Wanyama amepewa siku 90 kuondoka Amerika kwa hiari ama afurushwe kwa nguvu kwa mujibu wa sheria za uhamiaji za Amerika,” runinga hiyo ikamnukuu afisa mmoja wa idara ya uhamiaji akisema.

Wanyama, ambaye alisafiri Amerika kwa Visa ya mwanafunzi mnamo 1992 na akasoma mpaka akapata shahada ya uzamifu, atakuwa mwathiriwa wa hivi punde wa sheria kali za uhamiaji ambazo Rais Donald Trump anatekeleza.

 

You can share this post!

Wahadhiri waagizwa kurejea kazini Jumatatu au wafutwe

Canada yaitaka Kenya itoe sababu ya kumfurusha Miguna tena

adminleo