• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Mazingira ya biashara Kenya yainufaisha Huawei

Mazingira ya biashara Kenya yainufaisha Huawei

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya Huawei Technologies imepata faida kubwa baada ya kutoa matokeo yake ya kifedha, na kuonyesha kuwa kampuni hiyo inaendelea kukua.

Kampuni hiyo ilipata mapato ya dola 92.5 bilioni mwaka wa 2017, ongezeko la asilimia 15.7 ikilinganishwa na 2016.

Faida baada ya ushuru ilikuwa ni dola 7.3, ongezeko la asilimia 28.1. Kampuni hiyo ilitangaza kuwa ongezeko la mapato yanatokana na kuendelea kuimarika kwa soko la Kenya.

“Kwa kuzingatia uwezo wetu, tunashirikiana na wateja wetu ili kupunguza ufa kati ya wananchi walio na uwezo wa kutumia mawasiliano ya simu,” ilisema taarifa kutoka kwa kampuni hiyo.

Ilitangaza matokeo hayo huku ikiendelea kutekeleza suluhu ya kidijitali katika mfumo wa uchukuzi kupitia kwa reli mpya(SGR) kati ya Nairobi na Mombasa.

“Huawei inajikakamua kuhakikisha kuwa uchukuzi ni rahisi kwa watu na bidhaa. Tumejitolea kutoa miradi ya kibunifu (Smart) kwa wateja ili kuimarisha usalama wao, na kufanikisha uchukuzi pamoja na kuwapa abiria kumbukumbu kupitia kwa uchukuzi huo.

You can share this post!

Kutoa pesa ukitumia Paypal sasa utatozwa ada ya 1%

Sukari ya nje nchini yapungua pakubwa

adminleo