Kesi dhidi ya Mbogo yatupwa mlalamishi kukosa kufika kortini
Na RICHARD MUNGUTI
KESI ya ufisadi ya Sh22.3 milioni dhidi ya mwaniaji kiti cha ubunge cha Starehe aliyesyhindwa Steve Mbogo na raia wa Cameroun Harrison Gilbert ya ulaghai wa Sh22.3 milioni ilifutiliwa mbali baada ya mlalamishi kukataa kufika kortini kumpeleka mkewe kujifungua katika hospitali moja ya London.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotumwa kwa afisa anayechunguza kesi hiyo mlalamishi huyo Bw Faizal Ahmed alimpeleka mkewe hospitali ya Chalsea kusubiri kulazwa Aprili 18, 2018
Mbogo na Gilbert walishtakiwa kumlaghai Bw Ahmed mwenye maduka ya kuuza dhahabu Dubai $ 223,000 (KSh22.3million) wakimdanganya watamuuzia kilo 56 za dhahabu.
Bw Ahmed hakufika kortini kutoa ushahidi licha ya kujua kesi hiyo ilikuwa imeorodheshwa kusikizwa Alhamisi.
Mnamo Nobemba 7, 2017 mlalamishi alikataa kufika kortini pia kutoa ushahidi.
Hakimu mkuu katika mahakama ya Citi Roseline Oganyo aliamuru washtakiwa waachiliwe chini ya kifungu cha sheria nambari 202 kwa kukosekana ushahidi.
Kiongozi wa mashtaka Bw Willy Momanyi alisema Bw Ahmed alitumana ujumbe hangefika kortini kutoa ushahidi kwa vile “anampeleka mkewe mja mzito hospitali London mnamo Aprili 18, 2018.”
Lakini wakili Daniel Bosire anayewatetea washtakiwa aliomba kesi hiyo itupiliwe mbali kwa “ Bw Ahmed angelisafiri kutoa ushahidi kisha arudi kumpeleka mkewe hospitali.”
“Mlalamishi hataki kesi hii ikiendelea ndio sababu hakufika mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya washtakiwa. Naomba kesi hii itupiliwe mbali,” aliomba Bw Bosire.
Hakimu aliitupilia mbali kesi hiyo akisema “ mlalamishi hataki kesi aliyowashtaki Mbogo na Gilbert ikiamuliwa. Ameshindwa kufika kortini kutoa ushahidi. Haitaki hii kesi. Naitupilia mbali kesi chini ya kifungu