• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Kampuni ya kusambaza maji Mombasa yapinga madai ya mazingira duni

Kampuni ya kusambaza maji Mombasa yapinga madai ya mazingira duni

Na MISHI GONGO

KAMPUNI ya Usambazaji wa maji ya Mombasa (Mowasco) imepinga madai yaliyoibuliwa na baadhi ya wafanyakazi wanaolalamikia mazingira duni ya kufanyia kazi.

Mkurugenzi wa Mowasco Antony Njaramba amesema kampuni hiyo imejizatiti kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Bw Njaraba, kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwachochea wafanyakazi ambao sasa wanatishia kususia kazi.

Mojawapo ya masuala ambayo Njaramba amesema Bodi ya Usimamizi wa Kampuni hiyo imeshughulikia ni kuajiriwa kwa wafanyakazi 137 waliokuwa vibarua.

Njaramba anahisi kwamba tishio la kususia kazi la wafanyakazi hao lililotolewa Jumatatu, limesababishwa na hatua ya kampuni hiyo kuanza kutathmini utendakazi wa wafanyakazi hao.

“Kampuni imebaini kwamba baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakishirikiana na watu wanaojihusha na wizi wa maji,” amesema Bw Njaramba.

Kuhusu suala la wafanyakazi kulalamikia kutopandishwa vyeo na kutolipwa marupurupu jinsi inavyohitajika, Njaramba amesema tayari kampuni hiyo inayashughulikia masuala hayo.

Siku ya Jumatatu baadhi ya wafanyakazi walitoa notisi ya siku saba kwa kampuni hiyo kuzishughulikia changamoto mbalimbali walizoibua kuhusu mazingira magumu ya kufanyia kazi la sivyo wasusie kazi.

You can share this post!

Giza latanda Thika Road saa kadhaa

Maspika wa mabunge ya kaunti wataka kura ya maamuzi mwaka...

adminleo