• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 1:51 PM
Wawili wauawa na umeme Mukuru

Wawili wauawa na umeme Mukuru

Na SAMMY KIMATU

WATU wawili wamefariki baada ya kupigwa na stima umeme katika mitaa miwili ya Mukuru ilioko kaunti ya Nairobi Jumatatu. 

Mtoto wa mwaka mmoja na nusu alikufa baada ya kuteleza akicheza nje ya nyumba na kugusa waya.

Watoto waliokuwa wakicheza pamoja naye waliitana walipooana amekwa huku akiwa ameshikilia waya wa stima.

Kisa hiki kilitokea katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Hazina katika lokesheni ya Mukuru-Nyayo eneo la South B.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Bw David Kiarie alisema mtoto huyo alitambuliwa kama Yasin Mwathi Musyoka.

Majirani waliongeza kwamba mamake marehemu ni mwanafunzi wa kidato cha nne aliyemleta mtoto kuona babake kwa sababu wanafunzi walikuwa kwenye likizo ya wiki moja.

“Mama wa mtoto, Bi Jane Musyoki ni mwanafunzi wa kidato cha nne na alikuwa amemleta kijana kukutana na baba yake. Wanatoka mtaani Mukuru- Kwa Reuben katika kaunti ndogo ya Embakasi Kusini. Makao mashambani ni Wote katika kaunti ya Makueni,” Bw Kiarie alisema.

Katika kisa cha pili, mwanaume alipoteza maisha akiunganisha nyaya za runinga baada ya mlingoti kuguza waya wa stima uliopitishwa juu ya paa la nyumba yake.

Kisanga hiki kilitokea katika eneo la Mandazi road katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kaiyaba katika kaunti ndogo ya Starehe.

Bw Kiarie aliwakashifu watu wasiohitimu wanaounganisha stima kiholela na kuhatarisha maisha ya wakazi.

Aliiomba serikali kufufua mradi uliofadhiliwa na Benki la Dunia wa kuunganisha wakazi mitaani ya mabanda ya Nairobi na nguvu za umeme.

Mitaani, vifyaa vya stima kwenye visanduku vilivyokuwa vya mita na nyaya zilikuwa zimeibwa na kubakia milingoti pekee.

Wiki mbili zilizopita kampuni ya Kenya Power ikishirikiana na maafisa wa polisi waliondoa transfoma 15 kutoka kwa mtaa wa mabanda wa Mukuru – Lunga Lunga.

Vilevile, walitwaa zingine kutoka Mukuru-Sinai, Mukuru-kwa Reuben na zilizokuwa mkabala wa barabara ya Lunga Lunga sawia na barabara ya Entreprise zilizounganishwa mitaani.

You can share this post!

ANN NJOROGE: Filamu Kenya ina malipo duni lakini usife moyo

Usanii ulivyomsaidia kukwepa makundi ya uhalifu Nakuru

adminleo