• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 8:55 AM
Polisi kizimbani kwa madai ya kuua mtu wakati wa kafyu

Polisi kizimbani kwa madai ya kuua mtu wakati wa kafyu

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA wa Polisi alishtakiwa kwa mauaji ya mkazi wa mtaa wa Mathare, Kaunti ya Nairobi wakati wa kushika doria za kuzima watu kutembea saa za kafyu.

Konstebo Beckham Osoro Okwaru alifikishwa mbele ya Jaji Daniel Ogembo mnamo Ijumaa na kukanusha shtaka la kumuua Reuben Karani Kirinya.

Beckham, inadaiwa alimuua Kirinya mnamo Aprili 13 , 2020, katika mtaa wa Mathare Area IV, Nairobi.

Kiongozi wa mashtaka, Bi Gikuhi Gichuhi alieleza mahakama kwamba mshtakiwa amepimwa akili na kupatikana yuko na akili timamu.

Wakili Geoffrey Omenke, anayemwakilisha Beckham aliomba mahakama imwachilie kwa dhamana.

“Mshtakiwa ambaye ni afisa wa polisi alijisalimilisha baada ya mauaji ya Kirinya. Amekuwa akizuiliwa katika kituo cha Polisi cha Muthaiga tangu Aprili 13, 2020. Nimemkabidhi kiongozi wa mashtaka nakala ya ombi la dhamana. Naomba mahakama itusikize leo (Ijumaa),” alisema wakili Omenke.

Kiongozi wa mashtaka alithibitisha amekabidhiwa nakala ya ombi la dhamana ya mshtakiwa.

Aliomba mahakama impe muda asome nakala ya ombi hilo kisha asikizwe Mei 14, 2020.

Mahakama iliamuru mshtakiwa kurudishwa rumande hadi Alhamisi.

You can share this post!

Uchuuzi marufuku katika mitaa iliyofungwa

HAMNITISHI: Joho awajibu wakosoaji wake

adminleo