• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:10 PM
Kongamano la Ugatuzi: Wachuuzi na bodaboda walia kutengwa

Kongamano la Ugatuzi: Wachuuzi na bodaboda walia kutengwa

Na SHABAN MAKOKHA

WACHUUZI na wanabodaboda mjini Kakamega wamelalamika kwamba Kongamano la Ugatuzi linaloendelea katika Shule ya Upili ya Kakamega halijawafaidi kibiashara.

Kulingana na Kiongozi wao Saidi Opamo ambaye alizungumza na Taifa Leo, wachuuzi hao walilalamika kwamba wamezuiwa kufika eneo la kongamano kwa kukosa vibali.

“Sisi hatujahisi faida za kongamano hilo kibiashara kwa sababu wateja wetu ni wale wale,” akasema Bw Opamo.

Mwenzake Erick Akola ambaye huchuuza mizizi ya mti wa kiasili maarufu kama ‘Mukombero’ alisikitika kwamba ulinzi mkali kwa aliodhani wangekuwa wateja wake umemzuia kuwafikia.

Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa hapo awali alikuwa amesema kima cha kuanda kongamano hilo kilikuwa Sh200milioni na wenyeji wangepewa fursa ya kwanza kuwapa wageni huduma bora ili wafaidike.

 

You can share this post!

Majambazi wanawake ‘Wakware Babies’ waibuka...

Matibabu ya bure katika hospitali ya Matiba

adminleo