'Lamu wataka kafyu isiwaguse'
Na MISHI GONGO
LICHA ya Rais Uhuru Kenyatta kupunguza muda wa utekelezwaji wa kafyu, amri hiyo inaendelea kuzikandamiza sekta za biashara na utalii katika Kaunti ya Lamu, kwa mujibu wa baadhi ya wakazi.
Washikadau katika sekta hizo wanalalama kwamba kafyu inayoanza saa tatu za usiku hadi saa kumi alfajiri inawaathiri vibaya.
Kwa mujibu wa washikadau hao, amri hiyo ni yaukandamizaji kwani Kaunti hiyo haijarekodi kisa chochote cha virusi vya corona.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari washikadau hao ambao waliongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Utalii katika kaunti hiyo Ghalib Alwy wamemtaka Rais Kenyatta kuwaondolea wakazi wa Lamu amri hiyo.
Hili linajiri siku tatu baada ya Rais Kenyatta kupunguza muda wa utekelezwaji wa amri hiyo ambayo sasa inaanza saa tatu usiku hadi saa kumi afajiri ikilinganishwa na awali ambapo ilikuwa ikianza saa moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri.
Ustawi wa Kaunti ya Lamu hutegemea pakubwa sekta ya utalii.